Kuhimiza Kusimama Usiku wa Ramadhan

Kitabu: Subul as-Salam Sharh Buloogh al-Maram (سبل السلام شرح بلوغ المرام ـ الإمام الصنعاني)

Mwandishi: Imam as-San’aani (rahimahullah)

:: Kusimama usiku 29/30 ya Ramadhan katika ‘ibadah::

Pointi za ziada

Ndugu Muislamu Mtume ﷺ amehimiza kusimama kufanya ibada katika masiku ya Ramadhan. Na mtu akiendelea na imamu kuswali mpaka akamaliza huandikiwa thawabu za mtu aliyesimama usiku kucha.

Na ni juu ya maimamu kumcha Allah katika kuswalisha taraweh. Inafaa awachunge wanaomfuata asiwaendeshe mbio bila ya utulivu (tuma’nina) katika kusimama, kurukuu na kusujudu.


Na Mtume ﷺ alikuwa ni mwenye kupenda kheri zaidi na ni kielelezo chema lakini hakuzidisha zaidi ya rakaa kumi na moja sio katika Ramadhan wala masiku mengine. Na Mtume ﷺ aliswali na jamaa katika Ramadhan kisha akaacha kwa kuogopea isifaradhishwe.


Na iliyo swahihi kutoka kwa Amirul muuminiina ‘Umar ibnul Khatwab (radhiAllahu ‘anhu) ni kuwa alimuamrisha ‘Ubai ibn Ka’ab na Tamimi Daar waswalishe watu kwa rakaa kumi na moja na hii ndio idadi aliodumu nayo Mtumeﷺ na akafuata khalifa muongofu ‘Umar Ibnul khatwab ndio bora zaidi, na ikiwa mtu atazidisha kwa mapenzi yake hapingwi lakini asifanye haraka kama wanavyofanya maimamu wengi waleo katika misikiti zetu.

‘Subhanaka Allahumma wa bihamdika, ash-hadu an la ilaha illa Anta, astaghfiruka wa atubu ilaika 

(O Allah, You are free from every imperfection; praise be to You. I testify that there is no true god except You; I ask Your Pardon and turn to You in repentance)

Share this, BaarakAllah Feekum: [“One who guides to something good has a reward similar to that of its doer” – Saheeh Muslim Vo. 3, No. 4665]

The Most Comprehensive and Authentic Explaination of the Quran!
Tafsir Ibn Kahtir (10 Vol)
Purchase the complete Tafsir Ibn Kathir (10 Vol Abridged) By Dar-us-Salam Publications.