Ni lazima kwa msomaji kujipamba na adabu za kisomo ambazo anatakiwa kujipamba nazo ikiwa ni pamoja na:
1 – Kumtakasia nia Allaah (Ta´ala).
2 – Kusoma akiwa na twahara.
3 – Kutumia Siwaak.
Kufanya mambo hayo ni katika kuyaadhimisha maneno ya Allaah (´Azza wa Jall).
4 – Ni lazima kwake kusoma kwa kutamka. Ambaye atatosha kusoma kwa kuangalia peke yake hazingatiwi kasoma na hapati thawabu za kisomo.
5 – Ni lazima kwake kuyazingatia yale anayoyasoma. Kwa sababu hayo ni miongoni mwa malengo yanayotakiwa.
6 – Miongoni mwa adabu za kisomo ni msomaji asujudu pale atapoipitia Aayah ya kisomo ilihali ametawadha pasi na kujali ni wakati gani.
7 – Asisome kwa sauti kwa njia ya kwamba akawakera walioko pambizoni mwake. Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliikaa I´tikaaf msikitini. Akawasikia wakisoma kwa sauti za juu akiwa kwenye hema lake akafunua pazia na kusema: “Zindukeni! Nyote ni wenye kumng´oneza Mola Wenu. Kwa hivyo baadhi wasiwaudhi wengine na baadhi yenu wasiwanyanyulie wengine kisomo” au alisema “… katika swalah.” [Abu Daawuud (1332), an-Nasaa´iy katika ”al-Kabiyr” (07/288, 289) na Ahmad (18/392-393). al-Albaaniy amesema: ”Cheni ya wapokezi wake ni Swahiyh juu ya sharti za al-Bukhaariy na Muslim.” Tazama ”as-Swahiyhah” (04/134).]