Risalah: Dhikr Allah fi Ramadhan (Kukithirisha Kumtaja Allah Katika Mwezi wa Ramadhan)
Mhusika: Shaykh Muḥammad Saʻīd Raslān (hafidhahullah)
Nini Maana Ya ‘Itikaaf?
Imaam Ibn Baaz (Rahimahu Allaah) amesema:
Ni kujiweka faragha kwa ajili ya ‘ibaadah na kujipwekesha kwa Allaah kwayo. Na hii ndio kujipwekesha ki-shariy’ah. Na wengineo wakasema kuhusu maana ya I’tikaaf ni kukata mahusiano na kila kiumbe kwa yale yanayohusiana na kuwahudumia viumbe. [Majmu’w Al-Fataawaa (15/438)]
Imaam Ibn ‘Uthaymiyn (Rahimahu Allaah) amesema:
I’tikaaf ni mtu kujilazimisha kubakia Msikitini kwa ajili ya utiifu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta’aalaa), ili ajitenge na watu na ashughulike katika utiifu kwa Allaah na ajiweke faragha nayo. [Majmuw’ Al-Fataawaa (20/155)]