- Allaah ameziapia siku kumi hizi
- Siku za manufaa na kumdhukuru Allaah
- ‘Amali zake ni bora kuliko kwenda katika jihaad fiy sabiliLLaah
- ‘Ibaadah zote zimejumuika katika siku hizi
Ibn ‘Abbaas (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) ameahadithia kwamba Mtume (ﷺ) amesema: “Hakuna siku ambazo ‘amali njema zinazotendwa humo, zinapendwa mno na Allaah kama (‘amali zinazotendwa katika) siku kumi hizi.” Yaani: Siku kumi za mwanzo wa mwezi wa Dhul-Hijjah. Wakauliza: Ee Rasuli wa Allaah! Je, hata kuliko jihaad katika njia ya Allaah? Akajibu: “Hata Jihaad katika njia ya Allaah isipokuwa mtu aliyetoka (kwenda kupigana jihaad) mwenyewe na mali yake kisha kisirudi chochote katika hivyo.” [Al-Bukhaariy]