Kitabu: Al-Arba’uwn An-Nawawiyyah Hadeeth 18: Mche Allaah Popote Ulipo.
Imepokelewa kutoka kwa Abuu Dharr Jundub bin Junaadah Na Abuu ‘Abdir-Rahmaan Mu’aadh bin Jabal (Radhwiya Allaahu ‘anhumaa) kwamba Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ““Mche Allaah popote pale ulipo. Na fuatisha kitendo kiovu kwa kitendo kizuri ili kikifute (kilicho kiovu), na ishi na watu kwa tabia nzuri.” [At-Tirmidhiy na kasema ni Hadiyth Hasan. Na katika baadhi ya nukuu: Hasan Swahiyh]
Download: Bonyeza nukta tatu (three dots) ili kuweza kupata durus kwa simu yako.