Allaah (Jalla wa ´alaa) amesema kuhusu waja wake:
وَالَّذِينَ يَبِيتُونَ لِرَبِّهِمْ سُجَّدًا وَقِيَامًا
“Na wale wanaokesha usiku kwa ajili ya Mola wao wakisujudu na kusimama.” – Surah al-Furqan (25):64
Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa mara nyingi akiswali swalah ya usiku na akisema:
“Enyi watu! Enezeni salaam, lisheni chakula, waungeni ndugu na swalini usiku wakati watu wamelala ili muingie Peponi kwa usalama.” – {at-Tirmidhiy (2485), Ibn Maajah (3251) na Ahmad (23835). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy katika ”Swahiyh-ul-Jaami´” (7865).}