Imani inapanda na inashuka. Tawheed inapanda na inashuka. Kutukana upepo kunaipunguza imani kwa sababu upepo umeumbwa na Allah na ni wenye kuendeshwa. Unatumwa kwa kheri na shari. Hivyo hautakiwi kutukanwa. Badala yake muumini anatakiwa kutendea kazi yale aliyofundisha Mtume (ﷺ) katika Hadiyth:
Ubayd bin Ka´b (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kwamba Mtume wa Allaah (ﷺ) amesema:
“Msitukane upepo. Mtapoona mnachokichukia basi semeni:
اللَّهُمَّ إنا نسألك خيرها وخيرَ مَا فِيها وخيرَ ما أُرْسِلَتْ بِهِ وَ نعُوذُ بِكَ مِنْ شَرِّها وَشر مَا فِيهَا وشَرَّ ما أُرسلت به
“Ee Allaah! Tunakuomba kheri za upepo huu, kheri ya yale yaliyomo ndani yake na kheri ya yale yaliyoamrishwa kuvileta. Na tunajilinda Kwako kutokamana na shari ya upepo huu, shari ya yaliyomo ndani yake na shari ya yale yaliyoamrishwa kuvileta.”