Imaam al-Barbahaariy (Rahimahu Allaah) amesema:
Tambua kuwa Uislamu ndio Sunnah na Sunnah ndio Uislamu na kimoja katika hayo hakisimami isipokuwa kwa kingine.
Uislamu ni njia waliyokuja nayo Mitume (´alayhimus-Swalaatu was-Salaam). Mitume wote walikuja na Uislamu. Kila Mtume aliyelingania katika dini ya Allaah na akaja na Shari´ah kutoka kwa Allaah, basi huo ndio Uislamu. Uislamu ni kumuabudu Allaah (´Azza wa Jall) katika kila wakati kwa yale aliyoyaweka katika Shari´ah.