Siku ya Ijumaa ni siku adhimu kwa waislamu na fadhila zake ni nyingi. Kupata thawabu na malipo kwa kila hatua ya kwenda msikitini sawa na mtu aliyesimama kuswali na kufunga mwaka mzima. Amesema Mtume ﷺ:
“Mwenye kuoga na kujisafisha, kisha akaenda msikitini na mapema na akamkurubia khatibu na akasikiliza kwa utulivu. Mwenyezi Mungu ﷻ atamlipa kwa kila hatua malipo sawa na mtu aliyesimama kuswali na kufunga Mwaka mzima.” [Ahmad, At-Tirmidhi]