Salamu ni aina ya maamkizi ya Kiislamu na asili ya neno “Tahiyyat” yaani Maamkizi” linatokana na neno “Hayy” yaani hai” ikimaanisha kumtakia uhai na maisha yule anayesalimiwa. Ni ibadah kubwa kuwasalimia watu wa nyumbani mwako ukiingia nyumbani, na ni sunnah ya Mtume ﷺ kutoa salamu hata kama hakuna mtu nyumbani.